PAWASA ATOA USHAURI KWA TAIFA STAR. - LEKULE

Breaking

20 May 2015

PAWASA ATOA USHAURI KWA TAIFA STAR.


Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa Taifa Stars,BONIFACE PAWASA,amesema tatizo la nchi kutokuwa na mfumo mama wa soka litaendelea kulitafuna soka la Tanzania kwa kuendelea kutafuta mchawi kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo katika michuano mbalimbali.


Pawasa,ameiambia Chanel Ten Katika mahojiano maalum yaliyolenga kutaka kufahamu maoani yake kuhusiana na mchezo wa jana wa michuano ya COSAFA ambao Tanzania imepoteza bao 1-0 dhidi ya timu dhaifu ya Swaziland.

Amesema,nchi kama Ujerumani na Hispania zinatumia mfumo mmoja katika ligi za nchi hiyo hali inayosababisha wachezaji wa timu za taifa za nchi hizo kutokuwa na tatizo la kuzoea mfumo pindi wanapoitwa kutumikia nchi zao,amesema ni vigumu kwa wachezaji wa Taifa Stars kuzoea kwa muda mfupi mfumo wakataofundishwa na kocha yoyote kufutia hali hiyo.

Kuhusu mchezo wa jana Pawasa,katika maoni yake ameeleza kuridhishwa na namana chipukuzi wa Stars walivyocheza lakini amesema wameangushwa na uzoefu aidha amezungua tatizo la kucheka na nyavu ambapo amesema,litaendelea kuwa la kudumu iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa.Beki huyo Kisiki wa zamani wa Simba,amesema,takwimu katika misimu ya karibuni ya ligi kuu Bara,zimeonyesha kuwa wafungaji bora wa nafasi za juu ni raia wa kigeni.

No comments: