Osama:Mwandishi akanusha madai ya Marekani - LEKULE

Breaking

11 May 2015

Osama:Mwandishi akanusha madai ya Marekani


Mwaandishi mmoja mashuhuri kwa ripoti za upekuzi, Seymour Hersh, amekanusha madai ya utawala wa Rais Obama

kuhusiana na kuuawa kwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji la Al-Qaeda, Osama Bin Laden, nchini Pakistan miaka 8 iliyopita.

Akiandika katika jarida la London Review of Books, Bwana Hersh, alikanusha madai ya Washington kuwa, kutekwa na kisha kuuawa kwa kiongozi huyo wa AlQaeda ilikuwa ni janja janja za shirika la kijasusi la Marekani CIA.

Hersh anasema ukweli ni kuwa walisaidiwa pakubwa na shirika la kijasusi la Pakistani.

Aidha kiongozi mkuu wa kijasusi wa Pakistan anasemekana kuongoza mikakati ya operesheni hiyo ya kisiri.

Wakati ambapo Pakistan ilipojitenga na uvamizi huo na kuutaja kama ukiukaji wa uhuru na mipaka yake.

Marekani wala Pakistan hazijasema chochote hadi kufikia sasa.

No comments: