Hatua hiyo imekuja wakati ambapo viongozi wamekosolewa kwa kukaa kimya huku hali nchini Burundi ikizidi kuzorota.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania jana Jumatatu ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Burundi kimesema watu wapatao kumi na wawili wameuawa tangu maandamano kuanza tarehe 26 Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake tawala cha CNDD-FDD kugombea katika uchaguzi wa Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment