MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi GRC, Lusekelo Antony ‘Mzee wa Upako’ amekiri kushirikiana na waganga wa kienyeji kujipatia pesa kwa njia ya utapeli wakati akifanya biashara ya madini ya rubi.
Akizungumza katika ibada maalum hivi karibuni kanisani kwake Ubungo Kibangu jijini Dar, Lusekelo alisema utapeli huo aliufanya sehemu mbalimbali ikiwemo mkoani Dodoma kwa kuhusisha sangoma hao ambapo walikuwa wakimtaka mteja kuwapatia pesa huku wakimuelekeza mahali madini hayo yanapopatikana.
Alisema baada ya zoezi la kumuelekeza mteja, wao (Lusekelo na wenzake) walitengeneza kitu kinachofanana na madini hayo ambapo mteja hutoa pesa nyingi akiamini kuwa ni madini halisi.Kuhusu waganga hao, alisema walikuwa wakiwaandaa feki ambapo walimchukua mteja aliyehitaji madini hayo na kumtoza pesa nyingi ili mganga awaelekeze mahali yalipo na baada ya hapo huchukua yale madini feki kwa wingi na kwenda kuyaficha mahali ambapo mganga alimuelekeza mteja.
Alisema utapeli wa biashara ya madini ulimfikisha nchi mbalimbali duniani lakini Neno la Mungu lilipomfuata aliungama na kuanza kumtumikia yeye (Mungu).“Ulikuwa ni utapeli wa kiwango cha juu sana, kabla ya kufikia mafanikio maishani, watu hujikuta tukipitia njia zisizo halali. Msidanganywe na mtu yeyote, mafanikio ya kweli yanakuja kwa njia halali hadi sasa kila nikikumbuka huwa nasema Mungu anisaidie sana,” alisema Lusekelo.
Baada ya ibada hiyo, baadhi ya waumini walisikika wakiguna huku wakishangaa kusikia simulizi ya utapeli ya mchungaji wao.“Mmh, kumbe mtumishi amekutana na mapito mengi sana, hadi utapeli?” walisikika baadhi ya waumini wakati wakitoka kanisani hapo.
No comments:
Post a Comment