Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Guinea ,Moussa Dadis Camara ametangaza kwamba atawania urais wa taifa hilo baadaye mwaka huu.
Bwana Camara amekuwa akiishi mafichoni nchini Burkina Fasso baada ya kujeruhiwa katika jaribio la kumuua mwaka 2009.
Wakati wa uongozi wake ,takriban watu 160 waliuawa baada ya vikosi vya serikali kuwapiga risasi waandamanaji katika uwanja wa michezo wa mji mkuu wa Conakry.
Wiki iliopita wafuasi wa bwana Camara walifanya maandamano wakimtaka arudi nchini humo.
No comments:
Post a Comment