Michuano ya wavu Afrika Ijumaa- Mombasa - LEKULE

Breaking

8 May 2015

Michuano ya wavu Afrika Ijumaa- Mombasa


Michuano ya Afrika ya mpira wa wavu wa ufukuweni kwa wanawake yanaanza Ijumaa wiki hii katika Pwani ya Mombasa nchini Kenya.
Nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Burundi, Egypt, Kenya, Rwanda, Sudan, Tanzania na Uganda zinategemewa kushiriki kugombania nafasi nne kwa ajili ya kufuzu kucheza fainali za Michezo ya Afrika( All Africa Games) itakayofanyika nchini Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-19 mwaka huu.
Timu ya Tanzania imeondoka Dar es Salaam Alhamis kuelekea Mombasa kujiunga na timu nyingine zilizotegemewa kuwasili Mombasa mapema kwa ajili ya michuano hiyo.
Michuano hiyo ya wanawake inakuja miezi kadhaa baada ya ile ya wanaume iliyofanyika Dar es Salaam mwezi April ambapo timu za Rwanda ( walioibuka mabingwa), Burundi, Kenya na Misri kufuzu michezo ya Congo Brazzaville.
Shirikisho la mchezo huo barani Afrika (CAVB) hivi karibuni lilitaja kanda 7 za Afrika zitakazoshindana ili kutoa timu mbili kila kanda kwa ajili ya michezo hiyo mikubwa barani Afrika, ambapo zaidi ya wana michezo 3,000 watashindana katika michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, kuogelea na kukimbia (athletics).

No comments: