Marais wa Afrika wapinga kuondolea hatamu ya tatu - LEKULE

Breaking

20 May 2015

Marais wa Afrika wapinga kuondolea hatamu ya tatu

Viongozi wa Afrika Magharibi wamepinga pendekezo la kuondolewa kwa hatamu ya tatu .
Aidha marais wa Togo na Gambia wamepuzilia mbali pendekezo la kuondolewa kwa hatamu ya tatu.
Marais hao ambao walikutana katika hafla ya viongozi huko Ghana walikataa katakata kubadili katiba za mataifa yao ilikumruhusu rais kutawala kwa vipindi viwili na kisha aondoke madarakani ili mwengine achaguliwe.
Mataifa hayo mawili yanaruhusu rais kutawala hadi ataposhindwa.
Viongozi wengi barani Afrika wameibuka kuwa na kiu cha uongozi ,wengi wao wakikataa kuondoka madarakani hata baada ya kutawala muhula wa pili.
Viongozi wengi wamekuwa wakibadilisha katiba ilikuwaruhusu kuwania mihula ya tatu na zaidi kinyume na katiba.
Katika mataifa mengi swala la muhula wa tatu limeibua vurugu na maandamano.
Vurugu nchini Burkina Faso zimemsababisha rais kung'olewa madarakani.
Katika mataifa mengine kama vile Togo, maandamano hayakuweza kumng'oa rais madarakani .

Nchini burundi maandamano yanaendelea huku waandamanaji na rais Nkurunziza wakishikilia kukutu misimamo mikali .

Hata hivyo kuna baadhi ya viongozi ambao hawajatikiswa na wimbi la mabadiliko linaloendelea kuvumabarani Afrika.

Marais wa Zimbabwe, Angola na Guinea ya Ikweta wamekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya thelathini bila mipango yeyote ya kuachia ngazi.



No comments: