Waziri wa ulinzi wa Iraqi amesema
kwamba kiongozi wa pili wa ngazi ya juu katika mamlaka za kundi la
wanamgambo wa dola ya kiislamu IS, ameuawa katika mashambulio ya anga na
majeshi ya Marekani kwa kushirikiana na majeshi washirika.
Msemaji
wa wizara ya ulinzi wan chi hiyo, ameiambia BBC kuwa Abu Alaa al-Afari
aliuawa pamoja na seti kadhaa za wanamgamboa wa dola hiyo katika eneo la
Tal Afar lililoko kaskazini mwa nchi hiyo ya Iraq.Lakini waziri wa mambo ya ndani wa Iraq ametilia shaka juu ya kauli hiyo,nayo Marekani haijathibitisha juu ya kauli hiyo mpaka sasa.
Inaaminika kwamba Al-Afari alichukua madaraka ya kuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo la is wiki kadhaa baada ya kiongozi wao mkuu, Abu Bakr al-Baghdadi,kupata majeraha makubwa baada ya kushambuliwa kutokea angani .
No comments:
Post a Comment