CHADEMA yalia na sheria inayominya uhuru wa Habari - LEKULE

Breaking

25 May 2015

CHADEMA yalia na sheria inayominya uhuru wa Habari



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka watanzania kuipinga na kutoikubali sheria ya mpya iliyopitishwa ya takwimu kwa madai kwamba sheria hiyo inalenga kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na kuwanyima watanzania haki na uhuru wa kupata habari.

Akihutubia hivi karibuni mjini Bukoba katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk. Wilibroad Slaa alisema kupitishwa kwa sheria hiyo kunalenga kunyima uhuru wa habari pamoja na kuwafanya watanzania kuendelea kubaki gizani na kuishi kama wapo shimoni bila kuelewa maovu yanayofanywa na viongozi wasio waadilifu wanaotumia madaraka vibaya kwa masalahi yao binafsi.

Alisisitiza kuwa nia ya serikali kutaka kuzuia uhuru wa vyombo vya habari ni kuwarudisha nyuma watanzania ili waweze kuishi bila kupata habari kama ilivyokuwa enzi za ukoloni na kwamba hali hiyo haiwezi kuvumiliwa kwani serikali inataka kuficha maovu ambayo yanaweza kuliangamiza taifa hapo baadae.

No comments: