19:00 Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amewataka wahusika wakuu nchini Burundi kuweka uhasama baina yao kando ilikulinda taifa
18:55 Mwandishi wa BBC aliyeko Dar es Salaam anasema kuwa ndege ya rais Nkurunzinza imepaa ikielekea Bujumbura
18:53 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kufungwa kwa mipaka
18:45 Mwandishi wa BBC huko Bujumbura Kazungu Lozy anasema watu wangali wanasheherekea
18:40 Rais Nkurunzinza ameingia ndani ya gari lake na kuondoka mjini Dar es Salaam akionesha dalili kuwa yuaelekea Burundi
18:37 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi
18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe.
18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo
8:20 Generali aliyeongoza ''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo.
18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea
18:10 Esipisu amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta anaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba
18:07 Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema kuwa viongozi wanataka hali ya kawaida irejee huko Burundi
18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi
18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki
18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.
18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi
18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki
18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi
No comments:
Post a Comment