Kanisa la Kianglikana nchini
Uingereza linauza kampuni zake za uwekezaji zinazohusika na kuchimba
makaa, na changarawe kama hatua ya kuunga mkono juhudi za kupunguza
viwango vya hewa mkaa.
Kasisi Nick Holtham msemaji wa masuala ya
mazingira katika kanisa hilo amesema suala la mabadiliko ya tabia nchi
linafaa kujadiliwa na pande zote duniani.Hatua ya kanisa hilo itaathiri uwekezaji wake wa kima cha dola milioni 18.
Kanisa la Kiangilikana ya Uingereza lina uwekezaji wa dola bilioni 12.
No comments:
Post a Comment