Seleman
Msindi aka Afande Selle anawania kuwa mbunge mtarajiwa wa jimbo la
Morogoro Mjini kwa tiketi cha chama cha ACT Tanzania, na haogopi maneno
ya 'haters' wanaotaka kukiwekea mchanga kitumbua chake kwa mambo
yaliyopita.Bila shaka unakumbuka ile picha ambayo
Afande alipigwa akiwa amevua nguo na kubakia na boxer tu jukwaani wakati akitumbuiza!
Mfalme
huyo wa Rhymes anaamini kuwa picha haiwezi kumchafulia CV yake mbele ya
waajiri wake watarajiwa aka wananchi wa Morogoro Mjini.
"Hainiumizi, inanifurahisha," Afande aliiambia 255 ya XXL, Clouds FM.
"Inanifanya
nione kama namuenzi ipasavyo mfalme Daudi baba yake Suleiman.
Inanifanya niamini kwamba ufalme wangu haukuwa wa kubebwa.
Kwahiyo mpaka hapo inaashiria utashi wangu, hadhi yangu na ufalme wangu ambao leo hii unaenda kuwa ubunge wa Morogoro."
Unadhani Afande anaweza kuwa mbunge mzuri wa Morogoro Mjini?.
Unadhani Afande anaweza kuwa mbunge mzuri wa Morogoro Mjini?.
No comments:
Post a Comment