Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi ambao walimteka mlinzi na ndugu yake mmoja kisha kuwashushia kibano kikali huku wakiwaamuru wawapeleke kwenye chumba anacholala msanii huyo, Ijumaa Wikienda lina A-Z.
Mlango nyumbani kwa Alikiba ukionekana jinsi ulivyovunjwa na majambazi na kuiba vitu.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa na gazeti hili, Mei 2, mwaka huu, Abdul Kiba ambaye ni mdogo wa Ali Kiba, alisema usiku wa siku ya tukio alipewa taarifa na Ali Kiba kuwa amevamiwa na majambazi wenye silaha za moto hivyo alikurupuka moja kwa moja hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar ambapo waliripoti na baadaye kupata msaada wa polisi hadi eneo la tukio nyumbani kwa jamaa huyo Kunduchi Beach.
Sebuleni kwa Alikiba vitu vikiwa vimezaga zagaa baada ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa.
“Wakati linatokea tukio hilo nilikuwa Masaki (Dar) na jamaa yangu mmoja anaitwa Bude, kaka (Ali) alinipigia simu na kuniambia kilichotokea nasi hatukuchelewa tukaenda polisi na kuwaeleza hivyo tukaambatana nao hadi nyumbani.
Jamaa mmja ambae hakufahamika akikagua mlango wa chumbani jinsi ulivyovunjwa na kuchukua vitu.
“Tulikuta wamevunja mlango na kuzama ndani ambapo chumbani kwangu walichukua tivii flat screen, viatu na nguo zangu, maana kumbe wakati wanaenda chumbani kwangu walijua ni chumba cha Ali.
“Bahati nzuri majambazi walipofika walimwambia yule ndugu yetu aliyekuwa pamoja na mlinzi awaelekeze chumba cha Ali ambapo aliwapotosha kwa kuwaelekeza kwangu.
“Baada ya kuvunja mlango hawakumuona hivyo wakamuuliza akawaambia hajui labda katoka yeye akiwa amelala ndiyo wakaishia kuchukua vitu hivyo vya ndani.
“Wakati wanafanya hayo yote yeye (Ali Kiba) alikuwa akiwasikia tu chumbani kwake maana hadi wanatoka alikuwa akiwafuatilia kwa makini na hata maneno waliyokuwa wakizungumza yalikuwa yakutishia sana amani yake.
“Nashukuru kaka yangu hajaguswa, ila wameiba vitu kibao maana ukiachilia mbali tivii yangu na nguo wamechukua tivii ya sebuleni na kila kitu kilichobebeka,” alisema Abdul Kiba.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, jeshi la polisi lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa kuwasaka watuhumiwa.
Ni vyema mastaa mbalimbali ambao wanaonesha mali zao kama Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakaimairisha ulinzi nyumbani kwao ili kujilinda zaidi.
No comments:
Post a Comment