Watu 5 zaidi wauawa Afrika Kusini - LEKULE

Breaking

14 Apr 2015

Watu 5 zaidi wauawa Afrika Kusini


Watu watano zaidi wameuawa katika mashambulizi ya kibaguzi katika mji wa Durban nchini Africa Kusini.

Doria za maafisa wa polisi zimeimarishwa dhidi ya mashambulizi zaidi ya maduka yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya afrika.

Wengi wamelazimika kuhamia katika makaazi ya mda ,huku Malawi ikiripoti kuwaondoa raia wake ambao wameachwa bila makao.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshtumu mashambulizi hayo na kubuni kamati ya kujaribu kurejesha hali ya usalama.

No comments: