Watu 400 wafa maji wakielekea Italia - LEKULE

Breaking

15 Apr 2015

Watu 400 wafa maji wakielekea Italia


Kundi la wahamiaji manusura waliokolewa kutoka kwa bahari ya Mediterenia limewasili Italia.

Manusura hao walikuwa miongoni mwa wamiaji waliokuwa wakielekea bara Ulaya kabla ya boti lao kuzama na kuua zaidi ya watu mia nne.

Manusura hao wamepokelewa katika kisiwa cha Sicily na maafisa wa usalama na wale wa uhamiaji waliowapiga picha na kuchukua majina yao.

Awali Shirika la Umoja wa mataifa, lilitoa wito kwa juhudi zaidi zifanywe ili kuokoa maisha ya wahamiaji wanaojaribu kufika bara Ulaya kutokea Kazkazini mwa Afrika.

Zaidi ya wahamiaji 400 wanahofiwa kufa maji baada ya boti walilokuwa wakilitumia kuzama siku ya Jumatatu katika bahari ya Mediterenia.

Msemaji wa umoja wa mataifa anayejishughulika na wakimbizi Laurens Jolles ameiambia BBC kuwa, juhudi za sasa za kujaribu kuwaokoa wahamiaji ni chache mno.
Mwaka jana jumuia ya bara Ulaya yaliongeza operesheni ya uokoaji baharini, huku baadhi wakihoji kuwa huduma hizo zitachangia pakubwa idadi ya wahamiaji wanaovuka bahari na kuingia barani Ulaya.

Mwaandishi wa BBC katika kituo cha kuwahudumia wahamiaji Nchini Libya amesema kuwa kituo hicho kimejaa watu huku zaidi ya watu 500 wakitumia choo kimoja.

Watu hao walimuambia kuwa hali yao ni mbaya mno, na wanakusudia kuchukua njia hatari ya kuvuka bahari ili kuelekea Ulaya.

No comments: