Utawala nchini Indonesia unafanya maandalizi ya mwisho ya kuuawa kwa walanguzi tisa wa madawa ya kulevya, nane kati yao wakiwa ni raia wa kigeni.
Baadhi ya jamaa za watu hao tayari zimewasili kwenye gereza lililo kisiwani ambapo watu hao watauawa siku ya Jumatano.
Lakini wakati watapigwa risasi hakutakuwa mashahidi katika eneo hilo. Magari ya wagonjwa yaliyo na majeneza yamevuka kwenda kisia hicho .
Mapema waziri wa mashauri ya kigeni wa Australia Julie Bishop kwa mara nyingine aliitaka Indonesia kusitisha mauaji ya rai wawili wa Australia walio miongoni ya wale watauawa.
Lakini rais wa Indonesia Joko Widodo hajaonyesha dalili yoyote ya kuwapa msamaha watu hao.
No comments:
Post a Comment