Wahamiaji:Muungano wa Ulaya wapingwa - LEKULE

Breaking

24 Apr 2015

Wahamiaji:Muungano wa Ulaya wapingwa



Makundi ya kupigania haki za kibinadamu yamesema kuwa mikakati ilioafikiwa na muungano wa ulaya kuzuia idadi kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka hadi Ulaya kutoka Afrika sio ufumbuzi wa tatizo hilo.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika mjini Brussels siku ya alhamisi, Viongozi wa Ulaya walikubaliana kuongeza msaada wao mara tatu ili kuimarisha usakaji na uokozi wa wahamiaji katika bahari ya shamu.

Pia waliidhinisha mikakati ya kukamata na kuharibu vyombo vinavyotumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao.

Lakini Shirika la Human Rights Watch pamoja na lile la kuwasaidia watoto la Save the Children, yanasema kuwa EU inafaa kuongeza juhudi zake katika uokoaji badala ya kullinda mipaka yake.

Mkutano huo uliitishwa baada ya zaidi ya watu 800 kuuawa wikendi iliopita baada ya boti yao kuzama.

No comments: