Tishio la Ugaidi: Waziri Wa Mambo Ya Ndani Asema Nchi Ipo Katika Hali Ya Tahadhari - LEKULE

Breaking

7 Apr 2015

Tishio la Ugaidi: Waziri Wa Mambo Ya Ndani Asema Nchi Ipo Katika Hali Ya Tahadhari



Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Matthais Chikawe amesema nchi ipo katika tahadhari ya juu kufuatia taarifa za vyombo mbalimbali vya habari kwamba, kuna uwezekano wa shambilio la ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.

Chikawe amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya taarifa kusambaa kuwa mmoja ya waliokamatwa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ni Mtanzania.

Akiongea na BBC, Chikawe amesema mpaka sasa serikali bado haijaweza kuthibitisha ripoti hizo lakini vyombo vya dola nchi nzima viko macho na vimejitayarisha kwa lolote.

Pamoja na hayo waziri Chikawe amesema kuwa serikali inafahamu kuwa mmoja ya watuhumiwa walikokamatwa huko Garissa Kenya ni Mtanzania.

Hata hivyo amesema watawasiliana na polisi wa Kenya wakimaliza kumhoji mtuhumiwa huyo.

No comments: