Tishio La Ugaidi Kenya: Ziara Ya Miss World Nchini Humo Yapigwa Chini......Rais Obama Yeye Kasema Haogopi Kitu, Ziara Yake Iko Palepale - LEKULE

Breaking

8 Apr 2015

Tishio La Ugaidi Kenya: Ziara Ya Miss World Nchini Humo Yapigwa Chini......Rais Obama Yeye Kasema Haogopi Kitu, Ziara Yake Iko Palepale



Hali ya nchi ikiwa sio nzuri kuna vingi vinaathirika, unaweza ukaona kwa haraka haraka tu kwamba athari kubwa ni vifo na uharibifu wa mali za watu.. lakini ukiiangalia kiundani athari yake ni kubbwa zaidi ya hapo.

Rolene Strauss ni mrembo wa South Africa ambaye alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2014. Mrembo huyu alikuwa na ratiba ya ziara yake Nairobi Kenya na ilikuwa afanye hafla ya chakula cha usiku Nairobi March 10 2015.

Kutokana na ishu ya mashambulizi ambayo yametokea Chuo Kikuu cha Garissa Kenya, Rolene ameahirisha safari yake na amesema yeye pamoja na timu ya watu wake iliyokuwa aje nao Kenya watatangaza tarehe nyingine .

Kama hukujua ni kwamba mashambulizi ya Chuo hicho yamefanyika muda mfupi baada ya Rais Obama kutangaza kuwa atatembelea nchi hiyo July 2015.. Hata baada ya mashambulizi kutokea bado Obama amesema ratiba yake iko palepale.

No comments: