Shambulizi Garissa:Serikali yajitetea - LEKULE

Breaking

6 Apr 2015

Shambulizi Garissa:Serikali yajitetea


Serikali ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.

Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.
mwanajeshi wa KENYA.

Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi.

Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia.
WAJAESHI WA KENYA

Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na mwana wa chifu mmoja katika eneo la kazkazini mashariki.

No comments: