Polisi nchini Somalia wanasema kuwa takriban watu Saba wameuawa kwenye shambulizi lililolenga gari la Umoja wa Mataifa katika eno linalojisimamia la Puntland.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa linasema kuwa wanne kati ya wafanyikazi wake waliuawa wakati mlipuko mkubwa ulipolipua basi kwenye mji ulio kaskazini mashariki wa Garowe.
Shirika hilo linasema kuwa wale waliokufa wanatoka nchi tofauti. Kundi la wanamgamo wa Al shabaab linasema kuwa ndilo lililoendesha shambulizi hilo.
Al Shabaab limekuwa likiendesha harakati zake eneo la Puntland baada ya oparesheni iliyoendeshwa na vikosi vya Muungano wa Afrika mwaka uliopita ambapo waapiganaji wake walisukumwa kwenda maeneo ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment