Polisi Auawa na Wananchi Wenye Hasira Kali Mkoani Morogoro leo Mchana - LEKULE

Breaking

24 Apr 2015

Polisi Auawa na Wananchi Wenye Hasira Kali Mkoani Morogoro leo Mchana



Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, ameuawa leo mchana na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.

Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.

Mashuhuda wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

Baada ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo kumwua polisi mmoja.

No comments: