Nepal yakiri kulemewa na janga - LEKULE

Breaking

28 Apr 2015

Nepal yakiri kulemewa na janga


Serikali ya Nepal inasema kuwa imelemewa na kiwango cha janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi siku ya Jumamosi.

Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa vifaa na waokoaji.

Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya mahema , chakula na maji. Mwandishi wa BBC aliye kwenye kijiji kuliko kitovu cha tetemeko hilo, anasema kuwa zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa.

Zaidi ya watu 4000 wanathibitishwa kuaga dunia lakini waziri mkuu anasema kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

No comments: