Mwendesha mashtaka wa kituruki ambae alizuliwa mateka katika mahakama moja mjini Istanbul na wapiganaji wenye mrengo wa kushoto amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika mapigano ya risasi na polisi.
Mwendesha mashtaka huyo ambaye alikuwa anahusika na uchunguzi wa kina, alipigwa risasa mara kadhaa katika operasheni iliyofanywa na vikosi vya uturuki ya kumaliza uvamizi uliodumu kwa siku moja kotini hapo.
Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, amesema mwendesha mashtaka huyo amepoteza maisha licha ya jitihada za daktari za kumwokoa."Upasuaji ulianza saa mbili na dakika ishirini na tao na ulimalizika katika muda mfupi sana. Mwendesha mashitaka wetu aliumizwa vibaya sana na kukimbizwa hospitalini na nimezungumza na mganga mkuu. Pamoja na juhudi zote hizi,kwa bahati mbaya alipoteza maisha. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya mwendesha mashitaka Mehmet Selim Kiraz." amesema waziri mkuu Davutoglu.
Waziri mkuu Davutoglu amesema baadhi ya taratibu za kiusalama zitaangaliwa upya kutokana na hali ya utekaji. "Wakati tunaangalia majadiliano ambayo yamefanyika hivi karibuni katika muundo wa usalama, tukio hili linafungamanisha usalama na uhuru. Wakati wa mikutano na mazungumzo yetu tumeamua ufanyike uchunguzi wa kina kuhusu tukuio hili na kubaini kasoro za kiusalama. Tumeamuru hatua stahiki zichukuliwe katika siku za baadaye."
No comments:
Post a Comment