Mateka wa Mali aachiliwa huru - LEKULE

Breaking

6 Apr 2015

Mateka wa Mali aachiliwa huru


Jeshi maalum la Ufaransa nchini Mali limemwachilia huru mateka mmoja wa Uholanzi aliyetekwanyara miaka mitatu na nusu iliopita.

Wizara ya ulinzi nchini Paris imesema kuwa Sjaak Rijke aliokolewa wakati wa oparesheni kazkazini mwa Mali.

Wapiganaji kadhaa walikamatwa.

Hakuna tamko kuhusu hatma ya mateka wengine wawili ambao walitekwa wakati mmoja na Rijke wakati wa shambulio la wapiganaji katika hoteli moja huko Timbuktu mnamo mwezi Novemba mwaka 2011.

Bwana Rijke anadaiwa kuzuiliwa na wapiganaji wa Al Qaeda.

No comments: