WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, kukabidhi barabara ya magari yaendayo kasi kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART) ili zianze kutumika wakati sehemu zilizobaki zikiendelea kukamilika.
Hayo ameyazungumza Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli katika hafla uzinduzi wa barabara ya Uhuru ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam iliyofanyika leo katika viwanja vya Karume.
Pia Dkt. Magufuli amemwaagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo kasi(DART), Bi. Asteria Mlambo aharakishe kutafuta mabasi yaendayo kasi ili ifikapo Octoba Mwaka huu yawe yameanza kufanya kazi katika barabara ya Morogoro Road,jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick, amekemea vitendo vyote vya uhujumu wa miundombinu na uchafuzi wa mazingira ambavyo vinaathiri taswira ya jiji la Dar es salaam.
“Tatizo la wananchi wa Dar es salaam ni kutokutunza miundombinu pamoja na kutupa taka ovyo hali inayosababisha uharibifu wa miundombinu na kupelekea mafuriko wakati wa mvua”, alisema Meck Sadick.
No comments:
Post a Comment