Lipumba: Siku Ya Uchaguzi Mkuu Itatangazwa Na NEC Na Si Vinginevyo - LEKULE

Breaking

15 Apr 2015

Lipumba: Siku Ya Uchaguzi Mkuu Itatangazwa Na NEC Na Si Vinginevyo


Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na baraza la uongozi wa chama hicho (hawapo pichani) iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam, wapili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,Nassor Ahmed na kushoto ni makamu Mwenyekiti wa chama cha Wananchi (CUF) Taifa,Duni Haji.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akisikiliza kwa makini katika ufunguzi wa mkutano Baraza la uongozi wa chama wananchi (CUF) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Nassor Ahmed iliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Baraza la Uongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba (hayupo pichani) iliyofanyika jana Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.


TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ndiyo inayotakiwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu mwaka huu pamoja na kutangaza matokeo ya viongozi watakao kuwa wameshinda katika uchaguzi huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba wakati akifungua mkutano Baraza la uongozi wa chama hicho jana jijini Dar es salaam.

Lipumba alisema kuwa ucheleweshwaji wa uandikishaji wa daftari la wapiga kura linatia shaka kutokana na kutokukamilika kwa zoezi hilo mpaka sasa.

Aidha alisema kuna vifungu vya sheria kwenye katiba pendekezwa virekebishwe hasa kifungu cha Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) kutangaza Matokeo ya uchaguzi mkuu ya Rais atayekuwa ameshinda na awe amepata kura zaidi ya asilimia 50 pia matokeo hayo yahojiwe au yakikishwe na mahakama.

No comments: