Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
Pia Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Yaliokuwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni pamoja na kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Na serikali imetoa agizo Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na askari wa usalama barabarani wameagizwa kulifatilia hilo.
No comments:
Post a Comment