Kasi ya kujiunga na ugaidi yaongezeka - LEKULE

Breaking

2 Apr 2015

Kasi ya kujiunga na ugaidi yaongezeka



Zaidi ya wapiganaji wa kigeni elfu ishirini na watano kutoka mataifa mia moja walisafiri kwa nia na malengo ya kujiunga na makundi ya kijeshi kama al-Qaeda na Islamic State (IS), taarifa ya umoja wa mataifa imeeleza hayo.

Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba wapiganaji wageni ulimwenguni idadi yao imeongezeka mpaka kufikia asilimia sabini na moja katikati ya mwaka 2014 na march mwaka huu.

Nchi za Syria na Iraq ndizo nchi zinazolengwa kwa ukaribu zaidi na ndicho kitovu cha vijana wanaomaliza mazomo yao na kugeuka kuwa wenye msimamo mkali wa kidini.

Na pia taarifa hiyo imebainisha kuwa endapo kundi la IS lingeshindwa nchini Syria na Iraq,sasa wapiganaji hao kutoka nchi za kigeni wamesambaa ulimwenguni .

Nalo baraza la usalama la umoja wa mataifa liliwaomba wataalamu wa masula ya kijeshi miezi sita iliyopita kuchunguza vitisho vya askari wa kigeni wanaojiunga na kundi la Is na makundi mengine ya kigaidi.

Katika ripoti iliyowasilishwa kwenye baraza hilo mwishoni mwa mwezi uliopita ,na wataalamu wakaeleza kuwa ongezeko la wapiganaji wa nchi za kigeni zinazidi kuongezeka kulinganisha na muongo mmoja uliopita .

Maelfu ya wapiganaji wa kigeni ambao hufanya safari hadi nchini Syria ,Falme za Kiarabu na Iraq huko hufanya makao na kufanya kazi na kumalizia masomo ya elimu ya juu kwa wenye msimamo mkali kamalivyowahi kutokea kwatika nchi ya Afghanistan miaka ya 1990 .

Syria na Iraq inasemekana ina makaazi elfu ishirini na mbili kwa wapiganaji hao wa kigeni ,pia nchini Afghanistan makaazi elfu sita na mia tano na maelfu ya makaazi nchini Yemen, Libya, Pakistan na Somalia.

No comments: