Serikali ya Hong Kong imetangaza mapendekezo kukusu kuchaguliwa kwa kiongozi wa eneo hilo mwaka 2017.
Licha ya kushuhudiwa maandamano barabarani ya kuitisha demokrasia zaidi na mazungumzo ya muda mrefu mipango hiyo inasalia kuwa sawa na ile iliyotangazwa na China mwaka uliopita.
Wenyeji wa Hong Kong watawapigia kura wagombea lakini wagombea hao watahitajika kuidhinishwa na kamati kutoka China.
Wagombea wa nafasi hiyo ni lazima wapate uungwaji mkono wa asilimia kubwa ya kamati ya uteuzi ambayo itawajumuisha wanachama wa chama cha kikomisti.
Hata hivyo mpango huo haukubaliki na baadhi ya wapiga kura nchini Hong Kong ambao wanataka uchaguzi wa wagombea ulio huru.
No comments:
Post a Comment