Kwa moyo mkunjufu kabisa, nina penda kuwapongeza sana 93.7 Efm Radio kwa kutimiza mwaka mmoja tangu waanze kurusha matangazo yao hewani. Nina sababu nyingi za kuwapongeza lakini wakati wa kugonga “glass za cheers” niseme hivi; Kwanza kama unatafuta mifano halisi ya ufafanuzi wa mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa (BRN) mimi nafikiri EFM ni mfano halisi.
Kwa nini nasema hivi? Ndani ya siku 365, radio mpya imeweza kufikia nafasi ya pili kwa kusikilizwa na nakupendwa jijini Dar es salaam kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Geo Poll. Lakini pia ukiangalia uongozi wa kituo hiki, ni vijana na kwa wastani umri wao ni miaka 35, huo ni mfano mzuri kwa vijana. Uongozi wa EFM kuanzia Mkurugenzi Mtendaji Francis Ciza (Majey), Geoffrey Ndawula, Dennis Ssebo, Dickson Ponela, Hamida Siu, Omar Ramadhan na Reuben Ndege hao wote ni vijana tunaoishi nao mtaani lakini wamethubutu na wameweza.
Sababu nyingine ya kuwapongeza leo 93.7 EFM kwa kutimiza mwaka mmoja ni jinsi walivyo buni vipindi vyao na sio ku “copy na ku paste!” Nani alijua kwamba michezo inaweza kurushwa hewani saa tatu asubuhi kila siku na kukubalika ? Sasa EFM wana Sports Headquarters kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, huu ni ubunifu na imekuwa ni imeleta changamoto sokoni.
No comments:
Post a Comment