Chanjo ya Malaria,nafuu kwa Watoto - LEKULE

Breaking

24 Apr 2015

Chanjo ya Malaria,nafuu kwa Watoto



Hatua za mwisho za majaribio za chanjo dhidi ya Malaria, ya kwanza kufikia hatua hii inaleta matumaini kuwa itawalinda mamilioni ya Watoto dhidi ya Malaria.

Lakini Majaribio kwa watoto 16,000 kutoka nchi saba za Afrika yameonyesha kuwa kuna mipaka katika matumizi ya dawa hizo na chanjo haifanyi kazi kwa watoto wachanga.

Baada ya Watoto kufikia umri wa miezi 5-17 walipewa dozi tatu za chanjo, Kinga ilifanya kazi mwilini kwa kiasi cha 45%.

Lakini wataalam wanasema hatua ya kuifikisha chanjo katika hatua hiyo ni kupiga hatua kubwa.

Data zilizochapishwa katika jarida moja la maswala ya kitabibu zinaonyesha mafanikio ya chanjo hiyo ni madogo mno kwa vichanga.

Wanasayansi wamekuwa wakifanyia kazi chanjo hiyo kwa zaidi ya miaka 20, lakini wachunguzi wa mambo wanaona kuwa bado kazi kubwa inahitajika.

RTS,S/AS01 ni Chanjo ya kwanza ya Malaria kufikia hatua za juu za majaribio.

kwa sasa hakuna chanjo yoyote dhidi ya Malaria iliyopatiwa kibali duniani.

Chanjo hizi zilitolewa katika nchi 11 ikiwemo Tanzania,Kenya,Burkina Faso, Gabon,Ghana,Malawi na Msumbiji.

No comments: