Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) Chasema Mgomo wa Madereva Kesho ni Batili.....Kimesema Wamiliki Hawataki Magari Yao Yatumike Kuwagombanisha Na Serikali - LEKULE

Breaking

9 Apr 2015

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) Chasema Mgomo wa Madereva Kesho ni Batili.....Kimesema Wamiliki Hawataki Magari Yao Yatumike Kuwagombanisha Na Serikali


Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania, TABOA kimesema mgomo wa madereva unaotarajiwa kuanza kesho ni batili.

Sababu kubwa ya madereva hao kugoma ni kuishinikiza serikali kuweka mfumo mzuri wa ajira na kupinga kanuni inayowataka kurudia kusoma katika chuo cha taifa cha usafirishaji,NIT kila leseni zao zinapokwisha muda.

Kwa mujibu wa TABOA, madereva waliopanga kugoma hawatambuliwi kisheria,kwani wapo waliofukuzwa kazi kutokana na sababu mbalimbali ikwamo kusababisha ajali na sasa hawana magari ya kuendesha.

Mwenyekiti wa TABOA Mkoa wa Dae es Salaam, Hamza Mringo amesema madereva wanaotambuliwa kihalali na mamlaka ya usafirishaji Nchi kavu na majini,SUMATRA hawajawahi kushiriki mgomo uliofanyika April mosi, na hawatashiriki kamwe.

"Madereva wetu hawawezi kugoma kwa sababu tunaamini kila kitu kinaamriwa kwa utaratibu,tumepanga kukutana na serikali tuone jinsi ya utekelezaji wa hiyo kanuni inayoleta shida.

"Baada ya kuongea na serikali tukaelewana,tutakuwa tayari kuwalipia madereva wetu kozi ambazo wao wanaziona ni kero...inaelekea mgomo huu unamkono wa mwanasiasa mmoja tunamjua," amesema Mringo

"Wao wana ajenda yao ya siri,sisi hatutaki magari yetu yatumike kama ngao ya kutugombanisha na serikali.

"Mbaya zaidi hizi vurugu zao wanataka kuzifanyia eneo letu la kazi ambalo tumekabidhiwa kihalali." Alisema

No comments: