Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia(TBL) na SUBMiller East Africa Operesheni, Roberto Jarrin, akiwasilisha Mada kwa Wahariri wa Vyombo vya habari nchini waliofanya ziara katika kiwanda cha Bia Tawi la Mbeya.
Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akitoa maelezo kuhusu kiwanda hicho kwa Wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini
Meneja wa Kampuni ya Vinywaji ya Konyagi(TDL) akifafanua jambo kwa Wahariri wa vyombo vya ha
AHARIRI 22 wa Vyombo vya habari mbali mbali nchini jana walifanya ziara kwenye Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) wakiongozwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF).
Katika ziara hiyo Wahariri hao walipata maelezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Roberto Jarrin kuhusu hali ya kibiashara ya kampuni hiyo pamoja na bidhaa zinazozalishwa kisha kutembelea mitambo ya kutengeneza Bia.
Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari aliwaambia Wahariri Changamoto ambazo Kiwanda hicho kinakabiliana nazo kuwa ni pamoja na umeme wa grid ya taifa kuwa na nguvu ndogo ya kutokutosha kuendesha mitambo, ubovu wa barabara ya kuingilia kiwandani pamoja na upatikanaji wa maji.
Akitoa Shukrani kwa niaba ya Wahariri, Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kubanda, aliishukuru Kampuni ya TBL kwa kuwathamini na kuwaalika katika ziara hiyo na kuongeza kuwa watakuwa mabalozi wazuri kutangaza hali halisi waliyoiona kiwandani hapo tofauti na maneno ya watu mitaani.
Alisema watu wengi hudhani mazingira ambayo vinywaji vinatengenezwa hayafai jambo ambalo sio la kweli kutokana na kujionea wenyewe mlolongo mzima tangu uoshaji wa chupa hadi kinywaji kinavyojazwa kuwa katika hali ya usafi.
Kwa upande wake Meneja uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Editha Mushi alisema lengo la kuwaalika Wahariri wa Vyombo vya habari ni kudumisha uhusiano baina ya TBL na Vyombo vya habari.
Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutoa mrejesho kwa jamii juu ya hali ya kibiashara ilivyosasa na awali kupitia kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ili iwe wazi kwa kila mtu.
No comments:
Post a Comment