Watu wasiofahamika mara moja wamuua kwa kumchinja mkazi wa kitongoji cha kanoge mkoani Tabora. - LEKULE

Breaking

15 Mar 2015

Watu wasiofahamika mara moja wamuua kwa kumchinja mkazi wa kitongoji cha kanoge mkoani Tabora.

Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumchinja mkazi wa kitongoji cha Kanoge kata ya Usisya wilayani Urambo mkoani Tabora.

Wakiongea na LEKULE Mwenyekiti wa serikali ya kujiji cha Mabunduru pampoja na ndugu marehemu wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo hicho , kwani baada ya kumuua katika nyumba yake,watu hao hawakuchukua  chochote.

Diwani wa kata ya Usisya bMheshimiwa JAFARI KANKILA amesema tukio hilo ni la pili la wanawake kuuawa kwa kuchinjwa na ameahidi kutoa zawadi ya shilingi laki mbili kwa atakayetoa taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi SUZAN KAGANDA, amemtaja marehemu kuwa AMINA YUSUPH aliyekuwa na umri wa miaka hamsini na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa mauaji hayo.

No comments: