
Wapatanishi wa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi wamesema kuwa hatua ya pande zote mbili kushindwa kuafikia suluhu haikubaliki kimaadili wala kisiasa.
Waziri mkuu nchini Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye ndio mwenyekiti wa shirika linalosimamia mazungumzo hayo amesema kuwa viongozi wa Sudan Kusini wameshindwa kuwaongoza raia wao.
Hatua hiyo amesema itazidisha mateso na vita.
Mgogoro huo wa miezi 14 nchini Sudan Kusini umesababisha mamiloni ya watu kuishi bila makao huku makumi ya maelfu wakiuawa.

Serikali ya rais Salva Kiir na waasi,wanaongozwa na Riek Machar walikosa kuafikia mapatano katika siku ya mwisho ya mazungumzo hayo nchini Ethiopia yanayosimamiwa na shirika la Igad.
Majadiliano ya siku ya ijumaa pia yalikamilika bila mwafaka wowote.


No comments:
Post a Comment