Wanawake wa Nyeri walia na Nyani - LEKULE

Breaking

11 Mar 2015

Wanawake wa Nyeri walia na Nyani


Wakaazi wa wa Endarasha, kaunti ya Nyeri, wanaishi kwa mashaka makubwa kutokana na Nyani na tumbili wanaofugwa katika hifadhi ya taifa la Kenya ambayo iko jirani na makaazi yao,ambao huwashambulia na kuwanyanyasa wanawake tu.

Mkaazi Esther Wangui anaeleza alichoshuhudia jana kwamba nyani na tumbili kutoka katika hifadhi ya taifa ya Aberdare , Magharibi ya kitongoji cha Kieni, wamekuwa wakivamia mashamba yao katika makundi ya nyani na tumbili wanaokadiriwa kufikia 50 kwa wakati mmoja.

Katika tukio la hivi karibuni mwanamke mmoja alishambuliwa na nyani wa kiume wapatao kumi .walikuwa na kitisho kikuu,hufungua midomo yao na kuunguruma huku wameshikilia tupu zao huku wakimtishia anaeleza mwanamke aitwaye Wangui.

Mwanamke mwingine alishambuliwa na kuvuliwa nguo zake wakati alipokuwa akijaribu kuwazuia nyani hao wasivamie shamba lake .

Na wanaume upande wao wanalielezeaje tukio hili? John Kariuki anasema kwamba jamii hiyo ya wanyama inazidi kuongezeka kwakuwa wanapata chakula cha bure kutoka mashambani na huko kwenye hifadhi hawapati chakula cha kutosha.

Jambo kubwa zaidi linalofanya wanyama hao waongezeke kwa kasi ni kwamba, mmoja wao akizaa huzaa pacha.na wanadamu si wengi kiasi hicho kijijini hapo,na wanajibidiisha zaidi katika kilimo lakini hawapati mazao ya kutosha,anaeleza Kariuki.

Endarasha Peter Kamau ametoa wito wa kutafutwa kwa suluhisho la haraka kabla wakaazi hao hawajachukua sheria mikononi mwao.

No comments: