UN Watu 6000 wameuawa Ukraine - LEKULE

Breaking

2 Mar 2015

UN Watu 6000 wameuawa Ukraine


Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 6000 wameuwa mashariki mwa Ukraine.

Kwenye ripoti yake ya hivi punde kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine.

Afisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa inasema kuwa mapigano ya hivi majuzi yamesababisa vifo vya mamia ya watu.

Ripoti hiyo inatoa picha kuhusu hali ilivyo mashariki mwa Ukraine ambapo mamia ya watu wameuwa kwa muda wa miezi miwili iliyopita na kufikisha idadi ya wau ambao wameuawa eneo hilo kuwa takriban watu 6000.

Maisha ya raia na miundo mbinu imeharibiwa ambapo wachunguzi wa Umoja wa mataifa wanasema kuwa mashambulizi ya makombora hasa eneo la Debaltseve, yamewalazimu maelefu ya watu kukimbilia usalama wao

wakikabiliwa na uhaba wa chakula , maji , vifaa vya joto na madawa.

Ripoti hiyo pia inaangazia kile inachokitaja kwa visa kuingizwa kwa silaha nzito kutoka Urusi kwenda kwa waasi mashariki mwaUkrain.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ni ya kati ya tarehe mosi mwezi desemba na kati kati ya mwezi Februari wakati usitishwaji mapigano ulistahili kutekelezwa .

No comments: