Twitter kupambana na watumiaji wabaya - LEKULE

Breaking

12 Mar 2015

Twitter kupambana na watumiaji wabaya

Mtandao wa Twitter umebadili sheria zake katika kuzuia watumiaji wake kuchapisha kile Picha na video chafu.

Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema ''Marufuku kuchapisha picha au video chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa bila ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na picha hizo''

Mwezi uliopita vitendo hivi vilitambulika kuwa makosa ya jinai uingereza na Wales.

Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji watakaobainika kukiuka masharti mapya ''Anuani zao zitafungiwa''

Watumiaji wanaopeleka malalamishi Twitter kuhusu picha na Video zilizochapishwa watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia Kampuni kuwa hawakuwahi kutoa idhini ili kuchapisha picha au video mtandaoni na kuonekana kwa hadhira.

Yeyote atakayebainika kuchapisha picha hizo kinyuma na utaratibu wa sheria hii mpya atatakiwa kufuta kwanza kabla ya kurejeshwa tena mtandaoni.

Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria ambayo mtuhumiwa atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka miwili gerezani.

Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi.

Majimbo kadhaa ya Marekani wameweka Sheria ya kupambana na vitendo hivi hasa California,Texas na Utah.

Mabadiliko haya ya twitter yamekuja baada ya Kampuni hiyo kukosolewa kuwa imekuwa haifanyi jitihada madhubuti dhidi ya matumizi mabaya ya mtandao unaofanywa na watumiaji wake.

No comments: