TIMES FM YATOA MASHUKA 200 HOSPITALI YA MWANANYAMALA - LEKULE

Breaking

7 Mar 2015

TIMES FM YATOA MASHUKA 200 HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times FM, Rehure Nyulawa (kushoto) akisoma hotuba fupi kuhusiana na lengo la kutoa msaada huo kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sophinias Ngonyani pamoja na wauguzi.

Jengo la wodi ya akina mama wajawazito.

Kushoto ni Nyaulawa akimkabidhi mganga mkuu shuka walizozitoa.

Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akizungumza jambo katika makabidhiano hayo.

Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania mwaka jana, Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla hiyo, kushoto ni mwongozaji wa Kampuni ya Maznat Bridal, Maza Sinare Mchome akishuhudia makabidhiano hayo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamara (wapili kulia), Sophinias Ngonyani akiwa na wauguzi wa hospitali hiyo.
Kushoto ni Idd Azzan akitandika kitanda katika wodi ya akina mama wajawazito baada ya kukabidhiwa.
Mtangazaji wa Kipindi cha Maskani cha Radio Times FM, Sandra Tema akizungumza na mmoja wa wajawazito akielezea furaha yake kwa kupewa msaada huo.


RADIO Times FM, kupitia kipindi chake cha Maskani, jana iliungana na wanawake wote duniani kuadhimisha sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ambazo kilele chake ni kesho, Machi 8 kwa kutoa msaada wa mashuka 200 katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Times FM, Rehure Nyaulawa, alisema ingawa sherehe za Siku ya Wanawake Kitaifa mwaka huu zinafanyika mkoani Morogoro, kwa kutambua umuhimu wa wanawake, wameona si vibaya kukabidhi zawadi hizo kwa wanawake wajawazito na watoto katika hospitali hiyo.

Aliongeza kuwa, Times FM imeona ni vyema kuonesha dhamira yake ya dhati ya kutambua umuhimu wa wanawake hasa kwenye kuboresha mazingira yao wakati wa kujifungua, jukumu ambalo ni zito na ukizingatia linakabiliwa na changamoto nyingi.

“Sisi kama Times tumeona ni vizuri kuonesha dhamira yetu ya kutambua umuhimu wa wanawake hasa kwenye kuboresha mazingira yao wakati wa kuleta viumbe vipya duniani, si kazi rahisi, tumeguswa tukaona tutoe hiki tulicho nacho,” alisema Nyaulawa.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Sophinias Ngonyani aliwapongenza Times FM kupitia kipindi chao cha Maskani akisema wamefanya jambo busara kuweza kuwakumbuka akina mama na watoto katika kipindi hiki cha kuelekea kilelele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
“Niwashukuru Times kwa mchango huu lakini pia niwakaribishe watu wengine wenye uwezo na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wajitolee, kutoa ni moyo,” alisema Sophinias.

No comments: