KITUO cha kukuza vipaji vya wasanii Bongo (THT) kwa ushirikiano na Kliniki ya Foreplan iliyo chini ya Dk. Mwaka, hivi kinatarajia kufanya semini ya kuwaelimisha wasanii na vijana juu ya afya na uzazi.
Akizungumza kwenye kikao na waandishi wa habari mapema leo, Mkurugenzi wa THT, Ruge Mutahaba, alisema kwa vile kituo hicho kiko mstari wa mbele katika kukuza kazi za vijana na wasanii, kimeamua pia kuangalia na kuwasaidia katika masuala ya afya zao.
“Kwa kawaida binadamu wote hata kama utakuwa na pesa au kipaji cha aina gani, kama huna afya nzuri huwezi kufikia ndoto zako hata siku moja. Kwa kutambua hilo, tumeona umuhimu wa kushirikiana na Dk. Mwaka ili kuwapatia elimu ya afya na uzazi wasanii wote wa THT, na wengine hapa nchini,” alisema Ruge.
No comments:
Post a Comment