Tanzania:DSE,Soko bora la Hisa Afrika - LEKULE

Breaking

10 Mar 2015

Tanzania:DSE,Soko bora la Hisa Afrika



Ushiriki wa uwekezaji mkubwa wa kigeni kwa mwaka 2014 uliyawezesha masoko ya hisa ya kikanda kuweka rekodi katika kupata mafanikio kwa wawekezaji wengi kupata marejesho mazuri, hususan Soko la Hisa la Dar es Salaam, DSE nchini Tanzania, lililotajwa kuwa soko bora la hisa kuliko yote barani Afrika kwa mwaka uliopita.

Kipimo cha kampuni za ndani kilipanda kwa asilimia 27 mwaka jana, kiwango ambacho ni cha juu kabisa katika Afrika.

Mwezi Agosti mwaka uliopita, Tanzania iliondoa kiwango cha mwisho cha asilimia 60 kwa wawekezaji wa nje, na kufanya hisa za baadhi ya kampuni kubwa kuliko zote na zenye kupata faida kubwa kupatikana kwa raia wasio Watanzania kwa mara ya kwanza katika miaka mingi iliyopita. Uingiaji wa fedha za kigeni kumeboresha ufanisi wa masoko ya hisa.

Kwa mujibu wa makampuni zinazoripoti habari za kifedha duniani, Bloomberg, CBS na Thomson-Reuters, Soko la Hisa la Misri lilishika nafasi ya pili kwa kipimo chake kikuu kufikia ongezeko la asilimia 31.6 wakati Soko la Hisa la Uganda, USE, lilibuka katika nafasi ya tatu kwa asilimia 26.5. Soko la Hisa la Nairobi, NSE, lilishika nafasi ya nne, liliporomoka na kuapata asilimia 19.2

Soko la Hisa la Tanzania, DSE pia lilikuwa soko bora kuliko yote ya hisa barani Afrika kwa upande wa mtaji wa soko, ambao ulikuwa kwa asilimia 40 kufikia dola za Kimarekani bilioni $12.04, wakati hisa za ndani zikipanda kwa asilimia 66 kwa mwaka huo.

Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, DSE, Moremi Marwa amesema matokeo hayo yameonyesha imani kubwa ya wawekezaji katika soko la DSE kulikosababishwa na kuwepo mageuzi ambayo yana faida kwa uchumi wa Tanzania.

"Tuliweza kuwavutia wawekezaji wa nje katika soko hili walioshiriki katika soko lisilo na riba ya kudumu na upande wa mapato kamili ya soko letu. Pia tulianzisha mtandao wa WAN, ambao umeruhusu madalali kuingia katika miundombinu ya biashara na miamala na kuongeza saa za biashara," amesema Bwana Marwa.

Mwaka uliopita, Tanzania ilishuhudia kiwango chake kilichoorodheshwa cha soko kikipanda kwa soko la hisa kuweza kusajili kampuni tatu za ndani na nyingine kutoka Kenya.

"Mwaka 2014, tulifanikiwa kuorodhesha kampuni ya Maduka Uchumi kutoka soko la Hisa la Nairobi, Maendeleo Bank, Mkombozi Commercial Bank, na Swala Energy. Tunatarajia kuorodhesha kampuni tatu zaidi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, ambao mbili kati yake zitakuwa katika Soko la Ukuaji wa Kampuni na nyingine katika soko kuu," amesema Bwana Marwa.

Mwaka huo pia ulishuhudia kampuni zilizosajiliwa katika soko la hisa la DSE zikiongezeka kufikia 22, ambapo 14 kati yake ni za kutoka ndani, saba kutoka Soko la Hisa la Nairobi na moja kutoka Soko la Hisa la London.Mkurugenzi msaidizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Idara ya Masoko ya Ndani Paul Maganga amesema kuondoa kikomo cha mwekezaji wa nje kulikuwa na maana ya kuleta ushindani katika soko.

"Tunaangalia matokeo ya muundo wa sasa ili tuone uzito wa mahitaji ya dhamana za serikali yetu kutoka ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC. Mara tukifanya hivyo, tutaweza kufungua ushiriki katika masoko yetu kwa sehemui nyingine ya dunia," amesema Bwana Maganga.

Awali, Tanzania iliruhusu wawekezaji kutoka ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki tu, kununua dhamana za serikali kufikia asilimia 40 ya dhamana za serikali zilizowekwa katika soko kununua zaidi ya theluthi mbili ya mgawo wa asilimia 40.

Kampuni ya saruji ya Tanzania, kampuni ya pili kwa ukubwa ya utengenezaji saruji, ilikuwa moja ya kampuni zilizofanya vizuri kabisa ikipata marejesho ya asilimia 124.2 mwaka kwa mwaka. Kampuni nyingine zilizokuwa katika kiwango cha juu ni Twiga, ambayo ilipata asilimia 50; Kampuni ya Bia ya Tanzania,TBL, ambayo ilipata asilimia 76; CRDB Bank ilipata asilimia 54 ambapo kampuni ya Sigara ilipata asilimia 94. Swiss port ilipata asilimia 87, DCB Commercial Bank alipata asilimia 47 wakati ambapo Benki ya National Microfinance ilipata asilimia 30.

No comments: