Tanzania inapoteza mabilioni ya fedha kwa rushwa na udanganyifu unaofanywa na watumishi wa TRA - LEKULE

Breaking

2 Mar 2015

Tanzania inapoteza mabilioni ya fedha kwa rushwa na udanganyifu unaofanywa na watumishi wa TRA





Serikali imekiri kuwa Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kutokana na rushwa na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa mamlaka ya mapato (TRA) kwa kuvusha mizigo mikubwa bila kulipa kodi kwa kudanganya kuwa ni mali ghafi huku mingine ikidaiwa kupelekwa nje ya nchi na kuuzwa njiani hali inayo wafanya wananchi kukosa imani na taasisi za serikali.
Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora GEORGE MKUCHIKA ametoa kauli hiyo jiji Arusha alipokuwa anazungumza na watendaji wa mamlaka ya mapato takukuru na viongozi wa dini katika kikao cha mpango mkakati wa TRA kupambana na rushwa kwa kuwashirikisha wadau na kuongeza kuwa watanzania wamechoka kusikia upotevu wa mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya kunyakuliwa na watu wachache.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya amani ya viongozi wa dini SHEKH ALHAD MUSA amesema TRA imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi kuhusu kushamiri kwa rushwa hivyo kuna muhimu wa viongozi wa dini kutoa semina za neno la mungu kwa watumisi huku msaidizi wa askofu wa kanisa la KKKT Diosisi ya mashariki na pwani GEORGE FUPE akidai kabla kutengeneza mipango mkakati inapaswa kila mmoja ajitathimini kama inatosha kuwepo katika nafasi yake.

Kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini TRA, RISHED BADE amesema TRA ni taasisi iliyopo katika mazingira hatarishi kwa vishawishi vya rushwa lakini bado mikakati inafanyika kuondoa hali hiyo na sasa wameanza kushirikisha wadau katika kuianda mikakati mikakati hiyo.

No comments: