TAKWIMU KWA UFUPI KATIKA MCHEZO WA USIKU HUU WA LEO KATI YA MANCHESTER NA BARCELONA. - LEKULE

Breaking

18 Mar 2015

TAKWIMU KWA UFUPI KATIKA MCHEZO WA USIKU HUU WA LEO KATI YA MANCHESTER NA BARCELONA.


Katika kuelekea usikuwa Ulaya hii leo tukiwa na kumbukumbu nzuri Fc. Barcelona wameweza kushinda mara 17 ndani ya Champions Ligi na hii inaonesha kwamba wamefunga katika kila mechi ambayo wamecheza.

Muunganiko wa Messi, Neymar na Suarez umetengeneza magoli 15 ndani ya goli 17 ambapo kila mmoja ameweza kufunga goli ndani ya mechi 6 zilizopita katika katika michuao hiyo ya Ulaya.

Kwa upande mwingine Lionel Messi ambaye ndiyo amekuwa nyota wa Barcelona tunalinganishaje takwimu zake na mshabuliaji wa Manchester City Sergio Kun Arguero? Mchezaji ambaye atakuwa tegemeo katika ufungaji leo katika uwanja wa Camp Nou?

Watu hawa wawili Messi na Kun Arguero wana uwiano unaofanana katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Messi ana asilimia ya kufunga goli ndani ya dakika 75.8 huku Kun Arguero akiwa na dakika 76.5.

Licha ya hayo Manchester City watakuwa na Yaya Toure kiungo mmoja ambaye amekuwa tegemezi zaidi ndani ya timu hiyo, tuliweza kuona mchango wake mzuri sana ndani ya timu yake ya Taifa na kuisaidia kupata ubingwa wa kombe la Afrika

Endapo Manchester City watafanikiwa kuiondoa Fc. Barcelona leo katika uwanja wa Nou camp basi itakuwa ni timu ya tano ndani ya miaka 22 kuitoa Barcelona, kumbuka Real Madrid ndiyo waliitoa fc. Barcelona mwaka 2002 kisha Juventus mwaka 2003, Liverpool mwaka 2007 kisha Bayern Munich mwaka 2003.

Urejeo wa Yaya Toure unaweza kuwa na changamoto nzuri za kuwa na chachu ya ushindi ndani ya Camp Nou kutokana na umahiri wake wa kutengeneza nafasi za mwisho pia uwezo wake mzuri wa kucheza faulo na kupiga mashuti makali nje ya 18.

No comments: