SUGE KNIGHT AANGUKA MAHAKAMANI BAADA YA KUTAKIWA KUTOA SHILINGI BILIONI 45 KWA AJILI YA DHAMANA - LEKULE

Breaking

21 Mar 2015

SUGE KNIGHT AANGUKA MAHAKAMANI BAADA YA KUTAKIWA KUTOA SHILINGI BILIONI 45 KWA AJILI YA DHAMANA




Mwanzilishi wa Label ya Death Row, Mario "Suge" Knight jana alianguka mahakamani baada ya jaji kumtaka atoe dola milioni 25 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 45 za Kitanzania kwaajili ya dhamana kwenye kesi yake ya mauaji, kiwango ambacho wakili wake amesema ni kikubwa mno.

Wakili wa Suge, alisema mteja wake hawezi kumudu kulipa kiasi hicho cha fedha ambacho Suge aliishiwa nguvu na kuanguka dakika chache baada ya kusikia taarifa hizo akiwa mahakamani hapo.

Awali jaji huyo alidai kuwa ana wasiwasi Suge anaweza kutoroka kwa kuwa alishawahi kufanya hivyo siku za nyuma. Knight anashikiliwa kwa kosa la kuwagonga kwa gari watu wawili na kumuua mmoja baada ya kutokea malumbano.

No comments: