Serikali imeshauriwa kuwawajibisha na kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa kina, watumishi wake wote, wanaotuhumiwa kuhusika na uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambao wana hojiwa na kuchunguzwa, huku tayari chama cha mapinduzi kupitia kamati kuu kimewawajibisha viongozi waliohusika katika sakata hilo.
Akihutubia mamia ya wakazi wa Dodoma mjini na viunga vyake katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM taifa ndugu Abdulrahmn Kinana, amemshauri katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue kuwawajibisha ikiwemo kuwasimaisha kazi watumishi wa serikali waliotajwa kuhusika na akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha ndugu Kinana amekemea tabia ya viongozi wa serikali wanaoteuliwa kufanya sherehe ya kujipongeza, bila ya kutambua majukumu na mzigo unao wakibili, huku akisema kuwa, wananchi
Wamekuwa wakikerwa na tabia ya wizi wa mali za umma unaofanywa na watumishi wa umma bila ya kuwajibishwa kwa wanaotuhumiwa, na badala yake mwizi kupewa muda wa kujitetea huku kundi linguine likiibuka na kuanza kuwatetea wezi wa mali za umma na wasio na uadilifu.
Katibu mkuu huyo wa CCM taifa pia ameitaka serikali kuacha tabia ya matumizi mabaya ya fedha za umma kwa idara, taasisi na wizara kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwaajili ya kununua mafulana na kofia na kuwaagiza viongozi na wanachama wa CCM kutokaa kimya pale wanapoona serikali ikifanya vibaya na inapofanya vizuri waisifu, kwani mwisho lawama zote hugeukia chama cha mapinduzi kilichoomba kura kwa wananchi.
Kabla ya kuwahutubiwa wananchi katibu mkuu wa CCM taifa ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameongozana na katibu wa NEC itikadi na uenezi wa CCM taifa ndugu Nape Nnauye warishiriki kukagua na kuhimiza ukamiliswahi wa miradi ya maendelo ya wananchi na kuongea na wananchi waliojitokeza kumlaki kila kijiji alipokuwa msafara wake.
No comments:
Post a Comment