SEMINA YA UJASIRIAMALI KUFANYIKA 25-28 MACHI DAR LIVE - LEKULE

Breaking

19 Mar 2015

SEMINA YA UJASIRIAMALI KUFANYIKA 25-28 MACHI DAR LIVE

Mkurugenzi Mtendaji wa Ideal Healthcare Centre, John Kabugi (katikati), akielezea namna ya faida ya mti wa Mlonge ilivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fedha na Utawala wa Ideal Healthcare, Ester Mtwalizya, akizungumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani).(P.T)
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.
KAMPUNI Ya Ujasiriamali ya Ideal Healthcare Service Center inatarajiwa kuendesha semina kubwa ya siku nne juu ya ujasiriamali katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam tangu tarehe 25 hadi 28 Machi mwaka huu.
Akizungumza leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ideal Healthcare Service Center, John Kabugi , alisema katika semina hiyo ambayo kiingilio kitakuwa Sh. 10,000, watafundisha, miongoni mwa mambo mengine, jinsi mti wa Mlonge ulivyo bora katika biashara na manufaa mengine kwa binadamu. Hivyo aliwaomnba wananchi wajitokeze kwa wingi kunufaika na semina hiyo.
Alisisitiza kwamba mti wa Mlonge una faida nyingi zinaoufanya kuwa zao muhimu kwa Tanzania na nchi za nje kulingana na uzalishaji unaofanywa na kampuni yake.
Vilevile, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo tawi la Dar es Salaam, Salavai Izina, alisema semina hiyo itatoa mbinu mbalimbali za ujasiriamali kuhusu kilimo cha uyoga, ufugaji wa samaki na chakula chake , elimu ya masomo mbalimbali, mikopo na mitaji ya biashara, usindikaji wa mboga na matunda, na jinsi ya kuvikausha ili kuvihifadhi vitumike kwa muda mrefu.
Wakati wa semina kutakuwa pia na vitabu na CD za ujasiriamali ambavyo vitauzwa kwa Tsh.5000/=, ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya afya kupitia kwa madaktari wa Ideal Healthcare Wellness Centre.

No comments: