Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akimkabidhi Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori mkataba wa makubaliano ya kuanza kuendesha mfumo wa ukusanyaji wa mapato anayeshudia katikati ni Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. Makabidhiano hayo yamefanyika Morogoro
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akionesha mkataba walio saini na kampuni ya Selcom Tanzania baada ya kutiliana saini
kuanza kuendesha mfumo wa ukusanyaji wa mapato katikati ni Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. na Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori Makabidhiano hayo yamefanyika Morogoro
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kulia akitia saini mkataba
na kampuni ya Selcom Tanzania na
Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko, Juma Mgori katikati na kushoto n i
Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta
Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Mkurugenzi Mama Theresia Muhongo wageni waalikwa viongozi wa Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro itifaki imezingatiwa.
Awali ya yote kwanza kampuni ya Selcom inapenda kuwashukuru wote kwa jitihada zenu binafsi kwa kuwezesha Jambo hili linalofanyika leo hii litimie. Safari hii imeanza muda kidogo kuanzia kwenye mchakato wa tender hadi kufikia leo tuna sign mkataba kwa kweli kwanza tunapenda kumshukuru Mungu kwani ni yeye ndo ametuwezesha sote tufike hapa tulipofika leo. Na pia tunatoa shukrani zetu za dhati kwenu wote kwa kuonesha Imani kubwa kwetu sisi Selcom. Na tunawaahidi hatutawangusha hata kidogo tunapenda kuwajulisha kuwa chaguo lenu kwetu ni sahihi kabisa na hamtajutia hilo.
Baada ya neno hilo la shukrani napenda kidogo kueleza sisi Selcom ni nani?
Selcom ni kampuni ya kizawa na inayomilikiwa na Wazawa tena wazalendo na ilianzishwa mwaka 2001, na kuanzia kuanzishwa kwake tumejikita kwenye nyanja ya urahisishaji wa mifumo ya malipo kwa njia ya kieletroniki. Selcom ndiyo muuzaji namba moja wa mauzo yote ya LUKU nchini na mafanikio haya yamepatikana kutokana na ubora wa hali ya juu wa mifumo yetu. Selcom hivi sasa inajivunia kuwa na mawakala zaidi ya 8,000 nchini kote ambao wanatoa huduma kwa kutumia PoS zetu. Mbali ya PoS kampuni yetu ndiyo inaongoza nchini kwa kuunganisha huduma zake kwenye zaidi ya mabenki 30 nchini ambayo nayo yamerahisisha wateja wake kufanya manunuzi mbalimbali na hata malipo kwa kupitia mtandao wetu.
Mbali ya mabenki hayo 30 ambayo yanatumia mtandao wetu, Selcom pia inawezesha makampuni ya Tigo Pesa, Airtel Money na Mpesa kufanya manunuzi ya huduma ya LUKU. Hivyo mtumiaji wa simu anaponunua LUKU kutumia simu yake basi atambue anatumia huduma zetu.
Katika jitihada za kuwakwamua Watanzania hususani inapokuja kwenye suala la malipo hatukuishia hapo. Hivi karibuni Selcom tumezindua huduma zetu mpya za ATM na Selcom card chini ya brand ya Selcom Cashpoint na Selcom Paypoint. Kwenye ATM zetu mteja wetu ataweza kufanya miamala yote ya simu kwa mitandao yote pasipo usumbufu na kwa haraka na kwa kupitia card zetu mteja ataweza fanya malipo yote na pia kufanya miamala kwa kutoa au kutuma pesa kwenye mitandao yote.
Kama Selcom, hatukuishia hapo kupitia benki 30 ambazo zimeungana na mtandao wetu mteja, mbali ya kufanya manunuzi na malipo ya huduma mbalimbali ataweza kufanya miamala ya kutuma pesa, kuhamisha pesa bila kujali kama ni kutoka kwenye simu yake kwenda benki au kutoka benki kwenda kwenye simu yake.
Huduma zetu zimekuwa zikikuwa kwa kasi na idadi kubwa sasa ya Watanzania wamekuwa wakizitumia kila kukicha. Takwimu zinaonesha zaidi ya Watumiaji LAKI SITA wamekuwa wakitumia huduma zetu kila Siku hii ni kwa kufanya manunuzi au malipo mbalimbali na hii ni Baraka kubwa kwetu na ni kutokana na ubora na umahiri wa mtandao wetu.
Mtandao wetu umekuwa bora na ukitegemewa na wengi kutokana na ubora wake na kwamba Teknolojia iliyotumika imetengenezwa nchini na unaratibiwa hapa hapa nchini na Wataalamu ambao ni Watanzania wazalendo bila kutegemea kitu chochote kutoka nje. Na hii ndo Siri kubwa ya mafanikio yetu Selcom.
Leo kwa ushirikiano na Halmashauri ya Morogoro tunasaini mkataba ambao utaleta mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa Mapato kwa njia za kieletroniki. Tukiwa na Imani kwamba mifumo yetu ya ukusanyaji wa malipo itaiwezesha Halmashauri ya Morogoro kuongeza pato lake maradufu. Tunaanza na ukusanyaji wa kodi za Majengo, mabango, soko la Mawenzi, hospitali na zanahati za afya.
Huduma rasmi ya malipo kwenye sehemu zilizotajwa itaanza rasmi tarehe 1 ya mwezi Aprili. Kwa sasa hivi tutakuwa kwenye kipindi cha majaribio ambayo kwa kiasi Kiikubwa yatahusisha sehemu husika zilizotajwa.
Kwa wakazi wa Morogoro, Selcom imekuletea ajira mlangoni kwako kwa kuongeza fursa ya wewe kuwa wakala wetu na mjasiliamali ambaye utahusika moja kwa moja katika kusaidia makusanyo ya kodi na hapo hapo kujiongezea kipato. Kwa maelezo ya jinsi ya kuwa wakala wetu, tafadhali fika ofisini kwetu Mtaa wa Jamhuri au kwa kutupigia simu namba 0784 670 075 au wasiliana moja na moja na Aly Mbaga kwa simu namba 0719 325 335.
No comments:
Post a Comment