Samatta,Ulimwengu, kuikabili Malawi - LEKULE

Breaking

25 Mar 2015

Samatta,Ulimwengu, kuikabili Malawi

Wachezi wa kulipwa wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewasili nyumbani Tanzania kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Malawi (The Flames).
Mechi hiyo inatambuliwa na FIFA, ikiwa katika kalenda yake ya mechi za kirafiki zinazochezwa sehemu mbalimbali duniani. Mechi hiyo itachezwa Jumapili Machi 29 kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Samatta na Ulimwengu wanacheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya watu wa Kongo (DRC) na wanatarajiwa kuungana na kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar.
Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu, ambapo Yanga imeshinda 3-1.

No comments: