Ofisa wa Ikulu, Rajab Shaban (katikati) akitoka katika chumba cha mahojiano.
Tume ya Maadili, katikati ni Jaji Hamis Msumi.
Rajab Shaban akitoa ufafanuzi kuhusu kashfa ya kuingiziwa shilingi milioni 80 na James Rugemalira wa kampuni ya VIP.
OFISA wa Ikulu, Rajabu Shaaban, leo amehojiwa na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyo chini ya Mwenyekiti Jaji Hamis Msumi kuhusu sh. milioni 80 alizoingiziwa kwenye akaunti yake iliyo Mkombozi Bank kutoka kwa James Rugemalira. Kikao hicho kimeahirishwa hadi tarehe 13 mwaka huu ili mamlaka husika ziweze kutoa maamuzi.
No comments:
Post a Comment